https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, December 18, 2012

Kibanda aula New Habari 2006 Ltd



Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MHARIRI Mtendaji wa zamani wa Kampuni ya Free Media Ltd, inayochapisha gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda, leo ametangazwa rasmi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd.

Kibanda sasa anakuwa bosi wa waandishi wote katika kampuni hiyo inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African, iliyokuwa chini ya Mkurugenzi wake, Hussein Bashe.
Ofisa Mtendaji Mkuu, New Habari 2006 Ltd, Hussein Bashe

Akizungumzia ujio wake kwenye kampuni hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hussein Bashe, alisema Kibanda sasa ni mwenzao kwa ajili ya kuitumikia New Habari 2006 Ltd.

“Kuanzia leo tutakuwa pamoja na mwenzetu Kibanda katika kampuni hii na kushirikiana naye kiutendaji na majukumu yake,” alisema Bashe.

Naye Kibanda alisema alisema haoni sababu kwanini kampuni hiyo isipige hatua, hasa kutokana na rasirimali watu zilivyokuwa za kutosha.

Alisema kwa sababu hiyo, atashirikiana kwa karibu na wafanyakazi wote kwa ajili ya kusonga mbele na kuwa chumba cha habari chenye mafanikio makubwa nchini.

“Nashukuru sana, huku nikiamini kuwa tuliokuwa upande wa habari tunajua kwa dhati wakiwamo wahariri tunaokutana nao mara kwa mara kwenye shughuli zetu,” alisema Kibanda.

Kwa mujibu wa Kibanda, alikuwapo katika kampuni hiyo miaka 12 iliyopita wakati huo ikijulikana kama Habari Corporation.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...