https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, December 15, 2012

Waziri Sonyo awananga watunzi Tanzania




Waziri Sonyo, mwimbaji mpya wa Victoria Sound

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa dansi hapa nchini, Waziri Sonyo, amesema nyimbo nyingi zimekuwa nyepesi, jambo linaloweza kuangamiza soko la muziki huo nchini.

Sonyo aliyasema hayo mapema leo, ikiwa ni siku moja baada ya kutangaza kujiunga na bendi ya Victoria Sound, iliyokuwa chini ya Mwinjuma Muumini.

Akizungumzia hilo, mwimbaji huyo mwenye mwili mkubwa alisema kwamba nyimbo nyingi zimekuwa nyepesi na zinasababisha za zamani ziendelee kupendwa kuliko zao.

“Angalia nyimbo zao za leo utashangaa kwanini waimbaji na watunzi wamekuwa wakishindwa kuwaza na kupanga namna ya kutunga kazi bora.

“Nadhani hili litasababisha nyimbo kuwa mbaya na wadau hawawezi kuingiza mawazo yao moja kwa moja zaidi ya kuangalia kwenye Bongo Fleva,” alisema Sonyo.

Sonyo anayasema hayo, huku akiwa na changamoto kubwa ya kurudisha hadhi na heshima yake baada ya kupotea katika tasnia hiyo ya muziki wa dansi hapa nchini kwa miaka kadhaa.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...