https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, December 22, 2012

Rage azidi kusukiwa zengwe Simba


Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage (katikati), akifurahia jambo na mashabiki wa Yanga, jambo linalochukiza watu wa Simba.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa timu ya Simbaa, amezidi kusukiwa zengwe kwa madai kuwa anaipenda sana Yanga, huku akishiriki kwa wachezaji wao wengi kuuzwa Yanga, akiwamo Kelvin Yondan.

Wanachama zaidi ya kumi walizungumza na Handeni Kwetu, wakionyeshwa kukerwa na mwenendo wa mwenyekiti wao, hasa alipowaita wahuni walipotaka mkutano wa dharura kwa ajili ya kuangalia mustakabali wa klabu yao.

"Yule jamaa ni Yanga tangu zamani, hivyo vyovyo te vile, lazima afanye kazi kwa matakwa yake pamoja na faida ya timu yake, hivyo sisi wanachama lazima tuwe makini.

"Katika hali ya kawaida, hakuna mwenyekiti wa Simba aliyewahi kukutwa akifurahia kwa namna yoyote ile na watu wa Yanga, iwe ndani na nje ya nchi, huyu jamaa ni kibaraka wa jangwani,” alisema mwanachama huyo aliyeorodhesha jina lake na kufikia 698 kwa ajili ya kutakaa mkutano wa dharura waliyopanga ufanyike Desemba 30 Travertine Hoteli.

Handeni Kwetu ilitelewa picha zaidi ya tatu Rage akiwa na watu wa Yanga akifurahia nao, hata hivyo upo uwezekano mkubwa kuwa picha hizo zilipigwa walipokuwa wakikabidhiwa magari yao na wadhamini wao TBL.

Huo ni mwendelezo wa majanga yanayomuandama mwenyekiti huyo wa Simba, baada ya kuuwekea mizengwe mkutano huo wa dharura, akilinda kibarua chake.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...