https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, December 18, 2012

Mjasiriamali alia na mikopo Korogwe



Mama Kipande kushoto, mmiliki wa mgahawa unaofahamika kama (Mama Kipande), akiandaa kuku kwa ajili ya wateja wake, Manundu, wilayani Korogwe, mkoani Tanga juzi.

Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Korogwe
MJASIRIAMALI wa wilayani Korogwe mkoani Tanga, Zuhura Said maarufu kama (Mama Kipande), amesema kwamba kinachoogopesha watu kuhusu mikopo ni kutokana na masharti yake na usumbufu wake kwa ujumla.
Mama Kipande kama kawaida, akiandaa kwenye mgahawa wake
 
Mama Kipande aliyasema hayo juzi wilayani Korogwe alipotembelewa kwenye mgahawa wake wa ‘Mama Kipande’, maeneo ya Manundu kwa ajili ya kuangalia shughuli na changamoto zake.

Alisema watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na suala zima la mikopo, hivyo suala hilo linawafanya baadhi yao waone hakuna haja ya kujihusisha nayo.

“Ni mbaya kuona mtu anakimbia nyuma yake kwasababu alikopa, hasa baada ya kuona fedha zipo ingawa hana ndoto za kuziendeleza pesa za watu.

“Naomba serikali ijaribu kuangalia upya suala la mikopo ya nafuu kwa sisi watu wa kipato cha chini na sio kukopesha wale tu wenye viwanja au nyuma za thamani,” alisema.

Mama Kipande anafanya biashara ya mgahawa katika mji unaoendelea kwa kasi sana wilayani humo, huku kukiwa na mchanganyiko wa watu wengi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...