https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, December 12, 2012

Giraffe Ocean View wanavyojitolea kuendeleza sanaa





Mkurugenzi wa Giraffe Ocean View, Charles Bekoni

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIKA maendeleo ya sanaa yanayoendelea kutukia katika ardhi ya Tanzania, hakika yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano na moyo wa wadau wake.

Wadau hao wanafanya hivyo kwa kuamini kwamba itachangia kwa kuwakomboa wasanii na sanaa yao, jambo ambalo litawapa mwanga wa kujinufaisha.
Wapo wengi mno. Na kila mmoja ana umuhimu wake na nafasi yake, katika kuitangaa sanaa hiyo.

 Warembo wakijiachia katika hoteli ya Giraffe Ocean View, Dar es Salaam

Miongoni mwao ni Giraffe Ocean View Hoteli, iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, ambayo kwa hakika inafanya juhudi kubwa kuwasaidia sanaa na wasanii nchini.

Hiyo inatokana na hoteli hiyo kuweka utaratibu mzuri wa wasanii kupiga picha za kazi zao katika hoteli hiyo. Utaratibu huo kwa hakika unaleta tija.
 Warembo wakijiachia maeneo ya Giraffe Ocean View

Wasanii wanafanya mazuri kwa ushirikiano huo, ambao umewekwa na hoteli hiyo ya kisasa inayomilikiwa kwa kiasi kikubwa na Watanzania.

Katika sanaa ya maigizo, wasanii mbalimbali wamekuwa wakifanya sanaa zao hapo, hasa kwa kurekodi filamu zao hapo na kuwa kwenye kiwango cha juu mno.

Ukaicha wasanii wakubwa, hata wanaochipukia nao hawanyimwi fursa hiyo, ukizingatia kwamba lengo la hoteli hiyo ni kuwapa nafasi wasanii kuonyesha uwezo wao na kujipatia mafanikio.

Kwa kipindi kirefu mwaka jana, kundi la Dar Talents, maarufu pia kwa jina la Bongo Hood, lilikuwa likirusha mchezo wao wa Cinderela, ulioandaliwa kwa kiasi kikubwa na maeneo ya Giraffe.

Hii ni njia nzuri ya kuendeleza wasanii wachanga. Wasanii ambao kila kinachopita mbele yao, ni changamoto, inayoweza kuwakwamisha.

Wapo waliokuwa wakijidanganya kwamba ili uweze kurekodi katika hoteli mfano wa Giraffe, ni kuwa na jina kubwa au uwezo mkubwa wa kifedha.
Kama hao wapo basi wanajidanganya. 

Tena wataendelea kujidanganya, kama hawatatoa woga na kuamua kujitoa kama wanataka kufanya kazi nzuri.

Hoteli za kisasa, hasa zinazomilikiwa na Watanzania, zinaweza kuwasaidia Watanzania kwa ujumla, hasa kwa kuwashirikisha katika matukio makubwa ya kisanaa.

Huo ndio ukweli. Ukiangalia wasanii wakubwa waliofanikiwa hapa nchini, mara kadhaa hupenda kutumia hoteli hiyo kwakujua ni mahali pazuri.

Hata hivyo haitoshi, bado sanaa ya urembo nayo inategemea uwepo wa hoteli hiyo. Ingawa zipo hoteli nyingi hapa nchini, lakini kwao Giraffe wameona ndio kila kitu.

Inajitoa kwa moyo na nia ya kufanya nao kazi. Ndio, maana tunashuhudia ni jinsi gani Miss Tanzania, chini ya Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga, anapoitumia hoteli hiyo katika kuanbdaa shindano lenye mvuto.

Kwa miaka kaadhaa, Miss Tanzania wamekuwa wakiweka kambi yao hapo, ama kupata msaada wa aina mbalimbali, jambo linalotakiwa kupongezwa na wadau wote.

Mchango wao katika sanaa ya urembo ni mkubwa, huku nikiamini kwamba Miss Tanzania wasingeweza kuulipa kama wangetakiwa walipe kwa fedha.

Kila mmoja anafahamu gharama za kumlaza mrembo mmoja katika hoteli kubwa kama Giraffe Ocean View. Kama hivyo ndivyo, vipi kwa warembo wa Tanzania nzima wanaoshiriki shinda no hilo la kitaifa.

Ukiacha Miss Tanzania, ni Giraffe pia walioamua kulibeba kwa asilimia kubwa shindano la Unique Model.

Shindano hili lililoandaliwa kwa mara ya kwanza mwaka jana, liliweza kufikia hatua nzuri, baada ya kuwezeshwa kwa kiasi kikubwa na wadau hao wa Giraffe.

Kama hivyo ndivyo, ni vipi mimi kama mdau nitashindwa kutumia walau robo tu, kuwashukuru Giraffe Hoteli, chini ya Mkurugenzi wake, Charles Bekoni.

Hakika siwezi. Na kila mwenye nia ya kuitangaza vyema sanaa ya Tanzania, lazima atapenda kuwashukuru wadau hao, maana mchango wao ni mkubwa.

Bila hata kuangalia katika shindano la Dunia warembo wetu hupata kitu gani, ila katika ngazi ya kitaifa, hakika ni mchango mkubwa mno katika shindano la urembo.

Hivi karibuni, Mkurugenzi huyo wa Giraffe Ocean View, Bekoni, aliwahi kuliambia Handeni Kwetu kuwa lengo lao ni kuwapa mwanga na fursa wasanii wa Tanzania.

Hoteli hiyo itaendelea kuwaunga mkono wasanii na sanaa yao kwa pamoja, huku akisifia utaratibu huo kuwa ni sehemu ya kujitanua kibiashara.

“Biashara yetu inakuwa nzuri kama tutakuwa karibu na jamii, hivyo naamini bado tuna nia ya dhati ya kupiga hatua kutoka hii na kwenda nyingine.

“Naamini tutafanikisha ndoto zetu, ukizingatia kwamba tumepigania kuiweka hoteli hii katika kiwango cha juu mno kutokana na kujengwa vizuri pamoja na kutoa huduma nzuri na ya kuaminika,” alisema Bekoni.

Giraffe ni miongoni mwa hoteli za kisasa zinazowapa fursa wasanii kurekodi kazi zao, akiwamo marehumu Steven Kanumba, aliyefariki mapema mwaka huu.
0712 053949
0753 806087

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...