https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, December 18, 2012

Uchaguzi TWFA kufanyika kesho Morogoro

Zena Chande mwandishi wa Gazeti la Habari Leo, ni mgombea
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UCHAGUZI wa viongozi wapya wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) unafanyika kesho (Desemba 19 mwaka huu) kwenye hoteli ya Midlands mjini Morogoro.

Msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema Kamati ya Uchaguzi ya TWFA ikiongozwa na Mama Ombeni Zavala ndiyo itakayoendesha uchaguzi huo chini ya usimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Wagombea katika uchaguzi huo ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy wanaowania uenyekiti, Rose Kissiwa (mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (wanawania ukatibu mkuu).

Wengine ni Zena Chande (mgombea pekee wa nafasi ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...