https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, December 16, 2012

Watanzania wahimizwa wasikimbie kilimo


Meneja Mazao wa SASAMUA Estate, Josephat Odhiambo

Na Kambi Mbwana, aliyekuwa Handeni
MENEJA Mazao wa shamba la SASAMUA Estate, lililopo Kwamsisi, wilayani Handeni mkoani Tanga, Josephat Odhiambo, amewataka watu kuchangamkia fursa ya kilimo ili waweze kuinua uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Katika shamba hilo, mazao mbalimbali yanalimwa na kuuzwa ndani na nje ya nchi, zikiwamo nyanya, nanasi, mboga mboga na mengineyo, huku watu zaidi ya 2500 wakifanya kazi kwenye shamba hilo.

Akizungumza na Handeni Kwetu hivi karibuni katika shamba hilo, Odhiambo alisema kwamba bila kilimo uchumi wao hauwezi kukua zaidi ya kudidimia katika umasikini wa kujitakia wenyewe.

Alisema kilimo ni biashara nzuri inayoweza kuleta maendeleo makubwa, hivyo Watanzania na watu wa Handeni wanapaswa kuangalia kwa umakini ili wafanye kazi hiyo kwa malengo makubwa.

Nimetoka Kenya kuja kuifanya kazi hii katika shamba hili, nikiwa na imani kuwa tutauza na kufanya biashara nzuri ya kilimo, ukizingatia kwamba watu zaidi ya 2500 wanapata maisha kwa kufanya kazi hapa.

Naomba Watanzaniaa wafanye kazi ya kilimo kwa bidii kwa kuchangamkia ardhi ya kutosha na yenye rutuba, kwakuwa bila hivyo maendeleo kwao hayawezi kuwa mazuri zaidi ya kukaa kwenye ufukara wa kutisha,” alisema.

Hivi karibuni, Mkuu wa wilaya ya Handeni alifanya ziara katika shamba hilo akiwa na baadhi ya walimu wa shule za sekondari katika wilaya hiyo, paamoja na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali kwa ajili ya kujifunza kilimo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...