https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, December 23, 2012

Steve Nyerere apata kashfa nzito Bongo Movie




Steve Nyerere kulia akiwa na Wema Sepetu

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKALI wa filamu hapa nchini, Steve Nyerere amedaiwa kushika nafasi ya kwanza kwa wasanii wanaowaunganisha na mapedeshee warembo wanaofanikiwa katika game la filamu Bongo.

Kutajwa huko kumekuja wakati ambapo kashfa hiyo imezidi kushika nafasi katika sanaa, huku wadau wakisema Steve Nyerere ni kiboko kwa kuwaunganisha na watu wasanii wa kike.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu na msanii zinasema kwamba mkali huyo mwenye manjonjo mengi, alisema watu hao wamekuwa wakipitia zaidi kwa jamaa huyo ili wawanase warembo.

Alisema jambo hilo linamuweka katika mazingira magumu msanii huyo, ambaye anajulikana pia kwa uwezo wake kuigiza sauti za watu maarufu, akiwamo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

"Yule jamaa anajulikana kwa kazi hiyo, lakini sidhani kama ina ukweli hasa ukizingatia kwamba baadhi yao wanasema hivyo wakiangalia ukaribu wa msanii huyo na wasanii wa kike.

"Kwa mfano watu kutoka mikoani wenye uwezo mkubwa kifedha, wanadaiwa kuwa wakitaka ukaribu wa aina yoyote na wasanii wa kike wa Tanzania wenye majina hupitia kwake,” alisema mpashaji huyo ambaye naye alitembelea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wasanii hao wa Bongo Movie walipofanya ziara.

Kule mikoani, Steve Nyerere ndio alikuwa kinara wa kushika kipaza sauti na kuwaita wasanii waliokuwapo kwenye msafara huo wa Fiesta 2012, akiwawataka pia wacheze jukwaani.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...