https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, December 15, 2012

BAKWATA yazidi kurushiwa mawe na waislamu



Mufti Mkuu wa Tanzania, Shabaan Simba
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UMOJA wa Waadhir wa Kiislamu Tanzania, umesema kwamba mgogoro uliopo unatengenezwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, ili waendelee kuuza mali za Waislamu.

Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Umoja huo, Ustadh Said Juma Kinyogoly katika kutangaza juu ya kuwathamini na kuwaunga mkono viongozi wao, waliopatikana baada ya kufanya uchaguzi Novemba 20 mwaka huu.

Umoja huo ulichukua uamuzi baada ya kudai kuwa wapo baadhi ya watu wanaopita katika misikiti na kutangaza kuwa umoja huo haupo kihalali, jambo ambalo linaweza kuibua mgogoro mzito miongoni mwa waislamu.

Akizungumza mapema leo mchana, Msemaji wa Umoja huo, Kinyogoly, alisema kwamba BAKWATA wamekuwa wakifanya mambo ambayo ni mabaya kwa waislamu.

Hawa wamekuwa wakiuza mali za waislamu kwa faida yao, ukiwapo uwanja wa Markaz ambao kesi bado ipo Mahakamani.
 
Na sio heka tatu kama inavyojulikana, badala yake zipo heka 27 pamoja na nyumba mbalimbali ambazo kwa pamoja ni mali ya waislamu,” alisema Kinyogoly.

Kinyogoly pia alitumia muda huo kusema kuwa viongozi wao ni halali na wanaopita wakitukana wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.

Umoja huo upo chini ya Ustadh Habibu Mazinge aliyechaguliwa kuwa Amir Mkuu, Rajabu Juma, alishinda nafasi ya Naibu Amir Mkuu, Juma Ramadhani, Katibu Mkuu, ambaye hata hivyo alijitoa katika nafasi hiyo kutokana na kutingwa na mambo mengine, wakati Rashidi Piringu yeye alichaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Wengine walioshinda ni Mweka Hazina Mkuu, Hafidh Athuman, wakati Naibu wake ni Abdallah Mazrui, huku Hussein Feruzi akichaguliwa kuwa msemaji wa umoja huo, ingawa naye alijitoa, hivyo nafasi hiyo kubaki kwa Naibu wake, Kinyogoly.

Kwa mujibu wa Kinyogoly, wanaopita kuwasema vibaya viongozi wao, wautumie pia muda huo kuutetea uislamu pamoja na mali zake zinazouzwa kama njugu na viongozi kutoka BAKWATA pamoja na wanaoshirikiana nao kuudhoofisha uislamu.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...