https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, December 15, 2012

Rachel wa THT: 'Midume inapenda mauno yangu'



Rachel wa THT akiwa jukwaani akifanya vitu vyake
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKALI wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Winfirda Josephat maarufu kwa jina la 'Rachel wa THT', amesema kiuno chake kinawafanyua madume wamsumbuwe kila wakati, jambo analopambana nalo kwa kiasi kikubwa.

Katika nyimbo zake nyingi, ukiwamo ule wa 'Kizunguzungu' na sasa 'Nashukuru Umerudi' msanii huyo anafanya vitu vya aina yake, hasa kwa kunengua na kubinua macho yake, kama ilivyokuwa kwa msanii Ray C.

Rachel aliiambia Handeni Kwetu kuwa mauno yake yanawatoa udenda watu wenye matamanio, ingawa anakili kuwa usumbufu huo anakabiriana nao kwa spidi 120.

Alisema kwamba amekuwa akiwaza kitu kimoja tu ambacho ni muziki, hivyo wanaomtamani wafikirie zaidi kazi zake na sio mengineyo, hasa anapokuwa nje ya Dar es Salaam kwenye ziara zake za kikazi zaidi.

“Midume inatoa macho kwa mauno yangu, lakini ninachoangalia ni kazi yangu tu, hivyo hilo nimeamua kuliangalia kwa kina, ingawa naamini hao nao ni mashabiki wangu na wanapenda kipaji changu.

“Naamini nitafika mbali zaidi kwa kuhakikisha kuwa nina kazi nzuri na kuwapa burudani kamili mashabiki wangu katika shoo zote za ndani na nje ya Dar es Salaam, ukizingatia kwamba hiyo ndio ajira yangu na naamini mambo yatatakuwa mazuri,” alisema.

Recho kama anavyopenda kujiita anatokea katika taasisi ya kulea na kukuza vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), iliyoibua wasanii wengi wenye uwezo wa kutisha, akiwamo Linah, Barnabas, Amini na wengineo.
 

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...