https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, December 26, 2012

Arobaini ya sharomillionea Januari 4, 2013



Marehemu Sharomillionea, enzi za uhai wake
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
AROBAINI ya msanii wa vichekesho, marehemu Hussein Mkiety, maarufu kama ‘Sharomillionea’, inatarajiwa kufanyika Januari nne mwaka 2012 nyumbani kwao Lusanga, wilayani Muheza, mkoani Tanga.

Sharomillionea alikufa kwa ajali ya gari na kuacha huzuni kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa sanaa ya muziki na vichekesho hapa nchini, huku mazishi yake yakihudhuriwa na maelfu ya watu wa Tanga na nje ya jiji hilo la Wagosi wa Kaya.

Tangu alipofariki na kuzikwa Lusanga mwezi siku kadhaa zilizopita, wasanii wa vichekesho wamekuwa wakifanya vikao vya kila aina kwa ajili ya kumsaidia mama wa marehemu kijijini hapo na kuhitimisha arobaini ya nyota huyo.

Akizungumza na Handeni Kwetu, mmoja wa wasanii wa vichekesho, Fadhili Malidodi, maarufu kama (Defender), alikiri wasanii wa vichekesho kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kuweka mipango ya arobaini ya Sharomillionea.

“Tumekuwa tukikutana sisi kama wasanii wa Comedy kwa ajili ya kuangalia namna ya kumaliza tukio la nyota wetu, Sharomillionea aliyefariki kwa ajali ya gari nyumbani kwao Muheza, huku arobaini yake ikipangwa kufanyika Januari nne.

“Naamini Mungu akijalia tutamaliza na kuendelea kumlilia maana bado sisi tuliokuwa tunakutana naye mara kwa mara au kucheza naye kwenye filamu tunaendelea kuumizwa na tukio la kifo na mazishi yake kwa ujumla,” alisema Defender.

Wasanii wa vichekesho wameguswa sana na msiba huo kiasi cha kushiriki mazishi ya Sharomillionea kwa asilimia 100 tangu kifo chake na mazishi yake yaliyohudhuriwa pia na maelfu ya waombolezaji sehemu mbalimbali za nchi yetu.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...