https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, December 25, 2012

Jose Mara aipa masharti FM Academia

Jose Mara

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MWANAMUZIKI na mmoja wa wakurugenzi wa bendi ya Mapacha Watatu, Jose Mara, ameipa masharti bendi yake ya FM Academia, Wazee wa Ngwasuma kwa kuhakikisha kuwa hawaondoi picha yake kwenye mabango yanayoitangaza Ngwasuma, ingawa yupo nje ya bendi hiyo nchini.

Jose Mara kwa sasa ameondoka Ngwasuma na kufanya kazi na Mapacha Watatu, akiwa sambamba na Khalidi Chokoraa, huku wakiwa na pengo la Kalala Junior.
 
Akizungumza kwa hisia kali, Mara alimwambia mmoja wa mabosi wa Ngwasuma kuwa, sitaki nione mnaondoa sura yangu kwenye mabango yenu vinginevyo hata kuja kwenye shoo yenu itakuwa mwisho wangu,” alisema mwanamuziki huyo.

Ingawa Mara alisema kama utani, lakini sura yake ilitangaza ukweli halisi, hasa ukizingatia kwamba tangu aondoke kwenye bendi hiyo, lakini vipeperushi na mabango yanayotangaza kikosi cha maangamizi hakijabadilishwa kwa kiasi kikubwa.

“Hili bango nalipenda na kama siku nikiona limeondolewa basi utakuwa mwisho wangu kuja kwenye shoo ya Ngwasuma,” alisema Jose Mara, akilizungumzia bango lililowekwa nje ya New Msasani Club.

Jose Mara ni miongoni mwa vijana mahiri wa muziki wa dansi hapa nchini, akitokea kuwa na mashabiki wengi hapa nchini. Pia ni mmoja wa vijana wenye sauti jambo lililomfanya apate namba kila wimbo wa FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma.

Zipo habari zinazosema kuwa mwanamuziki huyo huenda akarudi Ngwasuma wakati wowote kutokana na maisha ya Mapacha Watatu kuwa ya kusua sua, hasa baada ya Kalala Junior naye kuamua kurudi Twanga Pepeta.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...