https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, December 22, 2012

Wagosi wa kaya kuvaana na Azam Uhai Cup



Baadhi ya wachezaji wanaounda timu ya vijana wa Azam FC



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU kutoka kwa Wagosi wa kaya, Coastal Union, imetinga hatua ya fainali na itavaana na Azam ya Dar es Salaam, katika michuano ya Uhai Cup, mchezo utakaopigwa kesho jioni, Desemba 23 katika Uwanja wa Karume.

Timu hizo zimepata fursa hiyo baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.

Azam ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata tiketi ya fainali baada ya kuitoa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mikwaju ya penalti 3-2. Matokeo ya dakika 90 yalikuwa bao 1-1, huku Coastal Union wakiivua ubingwa Simba kwa kuifunga mabao 2-1.

Mechi ya fainali itaanza saa 10 kamili jioni, na itatanguliwa na ile ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Mtibwa Sugar na Simba ambayo itachezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye uwanja huo huo.

Mbali ya kombe, bingwa wa michuano hiyo atapata sh. milioni 1.5, makamu bingwa sh. milioni 1 wakati mshindi wa tatu atajinyakulia sh. 500,000, huku timu iliyoonesha zaidi mchezo wa kiungwana (fair play) ikipata sh. 400,000 na mchezaji bora wa mashindano atapata sh. 350,000 wakati mfungaji bora sh. 300,000 na kipa bora sh. 300,000.

Aidha kocha bora katika mashindano hayo atazawadiwa sh. 300,000 kama itakavyokuwa kwa refa bora.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...