https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, December 25, 2012

Khadija Kopa kukamua Kivule leo

Khadija Kopa jukwaani

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MALKIA wa Mipasho nchini, Khadija Kopa na kundi lake cha Tanzania One Theatre (TOT)leo kitatoa shoo kabambe kusherekea sikukuu ya Krismas kwa wakazi wa Kata ya Kivule, Ilala kusherekea sikukuu ya Krismas kwenye ukumbi wa Vegetable Garden Pub.

Akizungumza mapema leo asubuhi, Kopa alisema kikundi hicho ambacho kitamba na nyimbo kemkem za taarab zinazotingisha katika miundoko ya Pwani ukiwemo Full Stop, Stop in Town na Mjini Chuo Kikuu ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki wake.

Alisema TOT taarab imesheheni kila idara ikiwa na wanamuziki wenye uwezo mkubwa wa kupiga taarab yenye mahadhi yanayokubalika akiwepo mkongwe Abdul Misambano, Mwanamtama Amir, Ali Star, Rukia Juma na Kopa Junior anayeimba nyimbo za Omar Kopa.

Mkurugenzi wa Vegetable Garden Pub, Anicety Mkwaya alisema maandalizi ya burudani hiyo imekamilika na zawadi zitatolewa kwa wale watakacheza taarab vizuri na watakaovaa vizuri.

Alisema burudani katika ukumbi huo zinaendelea ambako Januari 29 bendi ya Msondo Ngoma itatoa burudami katika ukumbi huo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...