https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, December 01, 2012

HelpAge na changamoto za Ukimwi duniani



 Meneja Mipango wa Shirika la HelpAge, Methew Kiongozi.
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
DUNIA nzima, leo inaadhimisha Siku ya Ukimwi duniani, ikikumbuka siku virusi vya ugonjwa huo vilivyogunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1983 na kuathiri watu wengi, zikiwamo nchi zisizokuwa na uchumi mkubwa.

Kitaifa, maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yalifanyika jana mkoani Lindi, huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na viongozi wengine wa serikali, akiwamo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi.

 Wazee wanaohitaji msaada wakiwa nje ya nyumba yao nchini Tanzania.

Maadhimisho hayo yanafanyika huku Taifa likiwa kwenye changamoto nyingi kutokana na watu wengi kuzidi kuambukizwa ugonjwa huo unaothiri pia nguvu kazi ya Taifa hapa hapa nchini, huku wakishirikishwa wadau wa afya na mashirika mengine yanayofanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya kuokoa nguvu kazi ya Taifa.

Miongoni mwa wadau hao ni Shirika la Kusaida Wazee la Help Age lenye makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, wakiingia kwenye kutoa elimu, kusaidia watu mbalimbali, wakiwamo wazee ambao wakati mwingine ndio wapo hatarini na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Watu wamekuwa wakikutwa na Virusi vya Ukimwi, hivyo kuonyesha kuwa bado kazi inahitajika kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo unaozidi kuathiri jamii na kupunguza nvugu ya Taifa.

Katika mazungumzo na MTANZANIA Jumapili, Meneja Mipango wa Shirika la HelpAge hapa nchini, Methew Kiongozi, anasema maadhimisho ya siku ya Ukimwi, yanaonyesha mikakati ya wadau wa afya kwa ajili ya kupingana na ugonjwa huo hapa nchini.

Anasema Desemba Mosi kila mwaka ni siku ambayo Watanzania wote wanaingia katika wakati wa kuangalia wapi wanatoka na wanapokwenda, huku elimu na jinsi ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ikizidi kutolewa kwa watu wote ili wafahamu changamoto hizo.

“Watanzania wote wanaingia katika kukumbuka waliokufa kwa ugonjwa wa Ukimwi na namna gani ya kutoa elimu ya maambuziki kwa watu ili wasiingie katika kuambukizwa zaidi ugonjwa huo hatari wa Ukimwi.

“Hapa nchini, maadhimisho yetu yalifanyika mkoani Lindi tukiwa na Rais Kikwete pamoja na Waziri wa Afya, Dk. Hussein Mwinyi, huku tukiamini kuwa tutatambua mbinu mpya za kupambana na Ukimwi na kuwakumbuka waliokufa kwa ugonjwa wa Ukimwi,” alisema Kiongozi.

Help Age inatambua kuwa Taifa linahitaji kupata ziro, yani kusiwe na maambukizi mapya, ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya UNAIDS kwa kukabiliana na VVU.

Lengo ni kufikia kizazi kisichokuwa na mtu aliyekufa kwa Ugonjwa wa Ukimwi au yule anayeugua ugonjwa huo kwa kuangalia mbinu na namna ya kuelimisha jamii na kutambua athari zake.

“Mbali na kukabiriana na maambukizi mapya ya Ugonjwa Ukimwi, pia tunahitaji kulinda haki za waliombukizwa tayari kwa kuweka sera nzuri.

“Kwa kufanya hivyo, tunatambua pia kuwa katika watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, wapo wazee wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, hivyo hatuwezi kuwasahau kwakuwa ni muhimu katika Taifa lolote kwa njia ile ile ya makundi mengine na idadi ya watu,” alisema.

Kiongozi anasema kwamba juhudi zinaonyesha kuwa mapambano ya Virusi vya Ukimwi yamewekwa zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 49 hivyo kuonyesha kuwa wazee wamekuwa hatarini sana kwa ugonjwa huo.

Zaidi ya asilimia 50 ya watoto yatima wa Tanzania, milioni mbili ni watoto wanaoishi katika mazingira magumu, huku ikitegemea wazee kufikia mahitaji yao ya chakula, afya na elimu.

Kwa mujibu wa takwimu iliyotolewa na Shirika la UNICEF lilieleza kuwa kwa mwaka 2007 tu, watoto waliofikia asilimia 40 kwa Tanzania walikuwa wakiishi kwa kutegemea babu na bibi zao.

Kiongozi anasema kwamba, kulingana na ripoti ya Ukimwi duniani, idadi ya watu wanaopata tiba ya kurefusha maisha (ART) uliongezeka kwa 63% ndani ya miezi 24.

Kusini mwa jangwa la Sahara, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 14 ya watu wote wanaoishi na VVU wana umri wa miaka 50 na zaidi, huku takwimu hizo zikitarajiwa kuendelea endapo juhudi hazitafuatwa na kupanda kwa uwezo wa watu 9,000,000 wakubwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi ifikapo mwaka 2040.

Athari za madawa ya kulevya za madawa ya kulevya zinachangia kwa kiasi kikubwa, ingawa upatikanaji wa dawa za kurefusha maisha unazidi kuwa rahisi zaidi, hivyo kuleta matumaini na furaha tele.

Kiongozi anasema ni watu wachache sana wasiopita asilimia 42.8 wanafahamu kuwa kwa kutumia kondomu pindi wanapojamiiana, wanaweza kujikinga na Virusi vya Ukimwi.

Juu ya unyanyapaa, matokeo hayo ya unyanyapa wa kijinsia kwa wanawake na wazee, bila kusahau hali ya VVU na nafasi zao za kiuchumi.

HelpAge na wazee kuwaita kwa ajili ya ukusanyaji, uchambuzi na kutoa data za VVU na UKIMWI zilizogawanywa kwa umri na jinsia kwa ajili ya watu wenye umri wa miaka 50 na zaidi.

Anasema kushughulikia kwa vitendo ukiukwaji wa haki za binadamu za wazee, wakiwamo wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi, wake kwa waume, ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti wa kuelewa mahitaji ya wazee.

HelpAge na watu wazee wanahamasisha huduma maridhawa kwa watu wazee ili kuhakikisha walioathirika wanapata kwa urahisi kinga, matibabu, matunzo na msaada ili kuishi kwa matumaini na VVU.

Itakuwa kuwa ngumu malengo ya kutokomeza ugonjwa huo ikiwa ripoti ya
2012 Global AIDS haitasema kitu kuhusu watu wazee na pia kushidwa kutambua uzee wa janga la VVU.

Kwa mujibu wa HelpAge, wazee wengi wamekuwa katika hatari ya ugumu wa maisha na maambukizi ya ugonjwa Ukimwi, jambo linalohitaji mipango, mikakati na sera madhubuti za kukabiriana na changamoto hizo.

Makala haya yameandikwa na Kambi Mbwana

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...