https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, December 01, 2012

Kilimanjaro Marathon yazinduliwa Moshi




MSIMU wa kumi na moja wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi 3, mwaka 2013, umezinduliwa mjini hapa juzi, katika Ukumbi wa Morio Hall, ikiwa ni dalili kuwa patashika hizo zitaanza katika Mkoa wa Kilimanjaro.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Leonidas Gama, wa pili kutoka kulia, akishuudia uzinduzi wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon, yaliyozinduliwa jana,  mkoani humo.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndiyo wadhamini wa mashindano hayo, George Kavishe, alisema wamedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika mbio hizo ili kuziendesha Kimataifa zaidi.

“Sisi kama wadhamini wakuu wa mbio hizi zinazoshirikisha wakimbiaji kutoka kila kona ya Dunia, tumedhamiria kuhakikisha tunaboresha mbio hizi na kuzifanya kuwa sura ya kimataifa,” alisema Kavishe

Alisema kutokana na matokeo ya mbio za mwaka huu, yaliyofanyika mapema Februari, na kushuhudia wakenya wakitawala mbio hizo, safari hii wamejipanga kwa kutoa changamoto ya zawadi zaidi ya kawaida kwa washindi.

“Tumeboresha mashindano nah ii ni kitu kipya , kwani kutokan ana aibu ya mashindano ya mwaka huu, mwaka ujao kila mshindi wa kwanza kutoka ndani ya nchi atapata maara mbili ya fedha za mshindi wa kwanza,” alisema Kavishe.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Dkt.Ibrahimu Msengi, aliwataka wanariadha wote watakaoshiriki kuhakikisha kuwa kile kilichotokea katika mashindano ya liyopita hasa ya mwaka huu yanbaki kuwa sehemu ya historia.

Alisema Mkoa umefurahishwa sana kuwepo kwa mashindano hayo mkoani hapa na antarajia mbio hizo zitachangia katika kukuza sekta ya Utalii, Uchumi na mahusiano ya kimataifa kutokana na kushirikisha wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali kutoka katika kila kona ya dunia.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa chama cha Riadha mkoani Kilimanjaro (KAA), Liston Nepacha alibainisha kuwa kwa kushirikiana na chama cha Riadha Taifa (RT), wamedhamiria kufuta mapungufu yote yaliyojitokeza katika mbio za mwaka huu na kuongeza kuwa tayari ya kikosi cha Tanzania kinaendelea na Maandalizi katika Kambi yao iliyopo Holili, Himo mkoani Hapa.

Mashindano ya Kilimanjaro Marathon yanayofanyika kila Mwaka yanadhaminiwa na Kilimanjaro premium Lager, Kilimanjaro Drinking Water, Arusha Hotel, Gapco wanaodhamini mbio za watu wenye Ulemavu, Bonite, Kiss Hotel, TPC, Shoprite, KK security, Simba Cement, Merenga Investment, CFAO Motors na yanatarajia kuwa na washiriki wapatao 6000.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...