Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
BENDI ya Extra Bongo,
imestushwa na kifo cha mpiga gitaa wa bendi ya WK sound, Joseph Watuguru, aliyefariki
juzi na kupangwa kuzikwa leo Kongowe jijini Dar es Salaam.
Marehemu Jose Watuguru kushoto enzi za uhai wake.
Watuguru aliwahi
kutamba na bendi kadhaa hapa nchini, ikiwamo ile Mchinga Sound akiwa na wakali
mbalimbali, hasa Mwinjuma Muumini maarufu kama kocha wa Dunia.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, alisema
kuwa kifo cha Watuguru ni pengo katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.
Alisema marehemu
alifariki kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya TB, huku akiacha mke na watoto
wawili na msiba wake upo nyumbani kwa kaka yake Kongowe.
“Watuguru ni miongoni
mwa wanamuziki waliokuwa na uwezo mkubwa hapa nchini, hivyo kifo chake ni pengo
katika ramani ya muziki huo na wengi tutamlilia.
“Mpiga gitaa huyo
mwenye uwezo wa aina yake amepangwa kuzikwa kesho, hivyo sisi kama Extra
Bongo, tumeguswa na msiba wake na hakika tutaendelea kumuombea mema zaidi huko
aendako,” alisema.
Mbali na Exta Bongo,
wadau na wanamuziki mbalimbali, akiwamo Muumini nao waliguswa na msiba huo
kiasi cha kumuongelea marehemu kutokana na kujadili kipaji chake kwenye kona ya
muziki.
No comments:
Post a Comment