Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
WANACHAMA
wa klabu ya Simba wa tawi la Mpira Pesa, wanatarajia kufanya mkutano Mkuu
Oktoba sita mwaka huu katika Ukumbi wa Anex Magomeni Mikumi, jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Mkutano
huo unafanyika kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoihusu klabu yao
wakiwa na lengo la kuhakikisha kuwa timu yao inafanya vizuri katika mechi za
Ligi Kuu.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tawi hilo la Mpira Pesa, Ustadh
Masoud, alisema kuwa maandalizi ya mkutano huo yanaendelea kwa ajili ya
kuufanikisha kwa vitendo.
Alisema
aidha pia watajaribu kuangalia namna gani tawi lao linaendelea kuwa na nguvu
katika tasnia ya mpira wa miguu hapa nchini ili mambo yao yaende vizuri.
“Tawi la
Mpira Pesa ni kati ya matawi yenye nguvu kwa klabu zote Tanzania, hususan Simba
ambao tupo zaidi ya wanachama 500 na wenye mapenzi ya dhati na soka letu
nchini.
“Tumeamua
tufanye mkutano wetu ili tuangalie namna gani ya kuitumikia klabu yetu ya Simba
kwa ajili ya kuendelea kufanya vyema katika soka na kuwa imara zaidi,” alisema.
Timu ya
Simba ambayo ipo kileleni kwenye msimamo wa ligi, inaongozwa na mwenyekiti wake
Ismail Aden Rage, ambaye mara kadhaa amekuwa akiwarushia makombora wanachama wa
Mpira Pesa kwa sababu mbalimbali na kuzua hofu kwa wanachama hao.
No comments:
Post a Comment