Na
Mwandishi Wetu, Handeni
KIVUMBI cha michuano ya kuwania Kombe la Mbunge wa Handeni, Abdallah Kigoda (Kigoda
Cup) kinatarajiwa kuanza kesho kwenye Uwanja wa Azimio wilayani humo
kikishirikisha timu 24 za soka na kumi za netiboli.
Kwa
mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo, Ahamadi Salehe Chihumpu, timu za Chanika
FC na Halmashauri FC zitafungua pazia la mashindano hayo upande wa soka, huku
Mdoe na Alfa na Omega zikikata utepe kwa netiboli.
Chihumpu,
alisema kuwa bingwa kwa upande wa soka atazawadiwa kombe na fedha taslimu sh
milioni 1, huku mshindi wa pili ataondoka na sh laki 5 na wa tatu sh laki 3.
Kwa upande wa netiboli, bingwa atabeba kombe na sh 300,000, wa pili sh 250,000
na wa tatu sh 200,000.
Mashindano
hayo yaliayoanzishwa na Kigoda, ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara,
yanalenga kukuza vipaji vya michezo kwa vijana wilayani humo, kuinua michezo na
kupata nyota wa kuunda timu bora ya wilaya ya soka na netiboli.
Chihumpu
alisema kuwa kabla Waziri Kigoda kuzindua rasmi mashindano hayo leo jioni, kutakuwa
na shamrashamra za ngoma za asili, dansi na shoo kutoka kwa wasanii mbalimbali
wa wilaya hiyo kuanzia saa 4 asubuhi.
Alisema
kuwa pia Waziri Kigoda atazindua rasmi ukarabati wa Uwanja wa Azimio
unaoendelea.
No comments:
Post a Comment