Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIPA wa timu ya Coastal Union ambaye kwa sasa mkataba wake
umefikia ukingoni, Shaban Kado, amewataka viongozi wa klabu yake kukaa ili
kumaliza tatizo la mgogoro liliojitokeza.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kado alisema kuwa
mgogoro huo unazungumzika ili kuisuka upya timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa
Ligi.
Alisema endapo uongozi utakaa chini kuangalia wapi wamekwama
na kwanini kumeibuka mzozo utakaoifanya Coastal ipoteze mwelekeo.
“Nimeishi Tanga kwa mapenzi makubwa kwa timu ya Coastal
Union, hivyo nadhani huu ni wakati wa kuzima mgogoro uliojitokeza kwakuwa
hautakuwa na tija.
“Mzozo unazungumzika kwa maslahi ya klabu hii yenye kuungwa
mkono na wadau wengi wa Tanga, jambo linalohitaji kuzimwa kwa mgogoro huu,”
alisema.
Kwa mujibu wa Kado ambaye mkataba wake umekwisha, mgogoro huo
ukiendelea inaweza kuleta tatizo kubwa katika mipango ya kimaendeleo ya klabu
hiyo.
No comments:
Post a Comment