Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU, mashabiki na baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba, wamejitokeza
kwa wingi kufunga ofisi za klabu hiyo kwa madai kuwa mgombea wao Michael
Wambura aneonewa na Kamati ya Uchaguzi inayoendesha mchakato wa Uchaguzi ndani
ya Simba.
Michael Wambura, pichani.
Wambura alikutana na waandishi wa habari, sambamba na
kutangaza nia yake kupinga uamuzi huo kwa Kamati ya Rufaa ndani ya Shirikisho
la Soka nchini (TFF), kwa madai kuwa mchakato mzima wa uchaguzi huo hauna lengo
zuri na upande wake.
Jengo la Makao Makuu ya Simba, likionekana kujaa watu waliokuwa wakisikiliza kinachoendelea baada ya mgombea Michael Wambura kuenguliwa katika mbio za kuwania urais wa klabu hiyo jana na Kamati ya Uchaguzi ya Simba.Akizungumza kwa umakini mkubwa, Wambura alisema Kamati hiyo haijamtendea haki kiasi cha kumuengua katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi ndani ya klabu yao ya Simba, ingawa mwenye anajua fika anayo haki na hadhi ya kuwania nafasi ya urais ndani ya Simba.
Alisema hajakubaliana na uamuzi huo, hivyo kesho saa 5
asubuhi atawasilisha rufaa yake katika ofisi za TFF, jijini Dar es Salaam. “Kuhusu uanachama wangu, niligombea nafasi ya Makamu wa Rais
wa TFF na nilipofika pale walinikatalia kuwa sio mwanachama wa Simba kwani
nilivuliwa uanchama tangu mwaka 2010 hivyo kutaka nipeleke barua ya utambulisho,
jambo ambalo klabu yangu ilinisaidia katika hilo,” alisema.
Aidha aliyataja majina saba ambayo hajakuwapo katika kikao
cha Kamati ya Utendaji ya Mei 5 mwaka 2010 kuwa hayajakuwapo kwenye kikao cha
kumfukuza uanachama wake, ingawa sahihi zao zinaonekana, hivyo zimefojiwa.
Majina hayo yaliyoandikwa kinyume na Omari Gumbo aliyekuwa
Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa kikao na wajumbe ni Idd Senkondo, Ayoub
Semvua, Abdalah Mkopi, Ramesh Patel, Hassan Hassan, Sultan Ahmed Salimu, Said
Rubeya na Yassin Mwete.
No comments:
Post a Comment