Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAKAMU
wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, amelipongeza Kanisa la Methodist Tanzania,
chini ya uongozi wa Baba Askofu Mkuu, Dkt. Byamungu kwa hatua nzuri ya
kuchangia harakati za kimaendeleo nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akimpongeza Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, baada ya kumkabidhi
Katiba na Kanuni za Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum
ya Kuwekwa Wakfu (kusimikwa) askofu huyo, iliyofanyika kwenye Kanisa la
Imanueli dhehebu la Methodox, Jimbo teule la Pwani na Mashariki
lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014. Picha na OMR.
Akizungumza
katika sherehe la kusimikwa Askofu Mteule Alen Siso, zilizofanyika Jimbo Teule
la Mashariki na Pwani, jijini Dar es Salaam, Dk Bilal alisema kuwa kanisa hilo
linapanuka sanjari na kuchangia mambo mengi ya kimaendeleo.
Alisema
kuwa Kanisa la Methodist Tanzania, lilianza kutoa huduma ya kiroho hapa nchini,
Juni 12 mwaka 1991 lakini ndani ya miaka 23 tu, limeweza kuchangia nyanja
mbalimbali za maendeleo ya jamii.
“Ujenzi wa hospitali tano mkoani Geita, shule mkoani
Arusha, uchimbaji visima virefu kwa shule na magereza katika mikoa ya Dar
es Salaam na Pwani, na ujenzi wa Chuo cha Theolojia huko Dodoma na
Arusha, ni baadhi tu ya mambo mengi mema, yanayofanywa na kanisa hili.
“Kwa
niaba ya Serikali, nawapongeza kwa kazi kubwa mnayofanya, huku nikiwataka
tuendelee kuwa karibu nanyi, kwa kila jambo mtakaloona tunapaswa
kushirikiana,” alisema.
No comments:
Post a Comment