Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI kwa kupitia Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki, imesema kwamba itazibana zaidi taasisi za kidini zinazofanya kazi zake
kiholela, ili kuepuka vurugu kwa baadhi ya taasisi zenye malengo tofauti.
Baadhi ya masheikh na wanazuoni wakiwa katika maandalizi ya kushiriki kongamano la umuhimu wa kutoa daawa (mihadhara), iliyofanyika katika Hoteli la Lamada.
Sadiki aliyasema hayo jana katika kongamano la Masheikh na
Wanazuoni lililofanyika katika Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam, lengo likiwa
ni kuwapa elimu na kujengewa uwezo wa kutoa daawa (mihadhara).
Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Masheikh na
Wanazuoni kwa kushirikiana na Kituo cha Kiislamu cha Misri, huku mgeni rasmi
akiwa ni Mkuu wa Mkoa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kwa ajili ya tukio hilo la aina yake.
No comments:
Post a Comment