https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Saturday, May 24, 2014

Kwakheri ya kuonana Amina Ngaluma, tutakukumbuka daimaNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi Tanzania, Amina Ngaluma, amezikwa leo mchana katika Makaburi ya Kitunda Machimbo, jijini Dar es Salaam, kuashiria kuwa sura au sauti ya mkali huyo haitasikika wala kuonekana tena ana kwa ana.
 

Kwakheri Amina Ngaluma, mwili wake ukiingizwa kaburini leo mchana, katika makaburi ya Kitunda Machimbo, jijini Dar es Salaam.
Ngaluma aliyefariki nchini Thailand, aliletwa jana usiku, ambapo wadau na mashabiki wa muziki wa dansi Tanzania, walipata fursa ya kushiriki katika mazishi yake.

Tofauti na wakati wa mapokezi ambapo wanaamuziki walishindwa kuhudhuria, jana katika mazishi hali ilikuwa nzuri kwa wadau wengi kujitokeza.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...