Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Uchaguzi Mkuu Simba umeanza kuibua hofu baada ya Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kuanza kuufuatilia kwa karibu uchaguzi
huo utakaofanyika Juni 29 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, baada ya maofisa wa
taasisi hiyo kuvamia bwalo la maofisa wa Polisi, jijini Dar es Salam, wakati wa
usaili wa wagombea.
Kuingia kwa maofisa hao, kumekuja huku uchaguzi wa Simba
unaotarajiwa kufanyika Juni 29 mwaka huu ukizidi kupamba moto na kila mmoja
kuwa na imani na mgombea wake kuwa ataibuka na ushindi.
Katika uchaguzi huo, nafasi ya urais inawaniwa na Evans
Aveva na Andrew Tupa, huku Michael
Wambura akitupwa nje hivyo kusubiri uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la
Soka nchini (TFF).
Mbali na urais, Swed Nkwabi na Godfrey Kaburu wanachuana
vikali, ambapo makundi ya wagombea hao wanaendelea kuchuana, huku kambi ya Nkwabi,
inaonekana kuwa na nguvu zaidi ya Kaburu.
No comments:
Post a Comment