NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MKALI wa sanaa ya maigizo ambaye pia ni mwongozaji wa tasnia
hiyo, Adam Kuambiana, amezikwa leo saa 9 alasiri katika makaburi ya Kinondoni,
jijini Dar es Salaam na kuacha simanzi kwa wadau na mashabiki wa sanaa hiyo.
Marehemu Kuambiana enzi za uhai wake.
Mazishi hayo yalitanguliwa na kuaga mwili wa marehemu
kulikofanyika katika viwanja vya Leaders Club, huku kibao akiwamo Waziri wa
Habari Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara kujitokeza katika mazishi hayo.
Kuambiana aliyefariki Jumamosi iliyopita, mwili wake
uliwasili mishale ya saa 4:30 katika viwanja vya Leaders kwa ajili ya kuwapa
fursa wadau, wasanii na mashabiki wa filamu kumuaga mkali huyo wa Regina, huku
akizikwa saa tisa alasiri.
Wasanii wengi walionyeshwa kupata majonzi, akiwamo Jacob
Stephen ambaye alishindwa kujizuia na kuanguka baada ya kushika kipaza sauti
kumuongelea marehemu.
Wasanii mbalimbali walipata nafasi ya kumzika msanii mwenzao
akiwamo Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Nisha, Mboto, Wakuvanga, Dkt Cheni, Muhogo
Mchungu na nyota wengine wote waliotokea Chama cha Waigizaji Tanzania (TFDA),
Shirikisho la Filamu Tanzania na muunganiko unaojulikana kama Bongo Movie
ambapo Stevu Nyerere ndio Rais wao.
Marehemu Kuambiana alifanikiwa kucheza filamu mbalimbali
kama vile Regina, Chaguo Langu, Mr Kadamanja, alizaliwa Juni 6 mwaka 1976,
Ifunda mkoani Iringa.
Wadau mbalimbali waliozungumza na Gazeti hili, walimuelezea
msanii huyo kuwa ni kati ya watu wanaoifanya tasnia ya filamu izidi kuheshimika
na kupendwa na wengi nchini.
No comments:
Post a Comment