Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama Cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna
Kibira, amelaumu wadau wa michezo kuelemea sana kwenye mpira wa miguu Tanzania.
Akizungumzia hilo, Kibira alisema kwamba katika tasnia ya
michezo yote, wadau wamekuwa wakiangalia zaidi mchezo wa kandanda, jambo ambalo
ni baya kwa maendeleo ya michezo mingine.
Alisema jambo hilo linasababisha kwa kiasi kikubwa kuharibu
michezo, hivyo serikali pamoja na wadau wote lazima waliangalie jambo hilo kwa
kina.
“Hii ni mbaya sana maana wenzetu wakitaka kufanya jambo lao,
linafanikiwa kwa haraka kwasababu wanapata msaada wowote wautakao.
“Sisi wa netiboli tunaona mpira wa miguu umezidi kutubana na
kutuweka katika mazingira magumu kupita kiasi, ingawa wote tunachangia kwa
kiasi kikubwa kukuza maendeleo ya michezo na kuitangaza Tanzania,” alisema
Kibira.
Kwa mujibu wa Kibira, kuna kila sababu ya wadau wote kuona
huu ni wakati wa kuungana kwa pamoja kuendeleza michezo yote, kama wanavyofanya
katika sekta ya mpira wa miguu.
No comments:
Post a Comment