https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, May 22, 2014

CCM yakuta malalamiko kibao jimbo la Tundu Lissu, Singida

Ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi ukiendelea katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu,ambaye anadaiwa kuwakataza  wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Mmoja wa Viongozi wa CCM,Wilaya akimpatia tofari Kinana walipokuwa wakisaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi, katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu. Mbunge huyo anadaiwa kuwakataza  wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo. Lakini baada ya kuona watoto wao wanateseka kwa kukosa elimu wananchi wameamua kupuuza katazo hilo na kuanza kujitolea kujenga vyumba hivyo vya madarasa.
Jengo la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kudaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya madaktari.
Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi nje ya engo la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kuaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya madaktari.
Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi, Unyaghumpi 
Wanafunzi wa elimu ya awali, wakifundishwa na mwalimu Juliana Joseph huku wakiwa wamekaa sakafuni na juu ya paa kukiwa wazi katika moja ya vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi, Unyaghumpi vilivyozuiliwa kujengwa na Mbunge Tundu Lissu kwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha na kuwaambia kuwa fedha zote zitatoka serikalini.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida,wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 

Katika Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge Tundu Lissu wa Chadema, Kinana alishuhudia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ujenzi wake umekwamishwa na mbunge huyo kwa kuwzuia wananchi kuchangia fedha za miradi hiyo akidai kuwa fedha zote zitatoka serikalini.

Baadhi ya miradi iliyosimama aliyoikagua Kinana, ni Zahanati ya Kimbwi ukiwemo ujenzi wa nyumba za waganga ambayo imeishia kwa kupigwa msingi wa zege. Vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Unyaghumpi ambapo walikutwa watoto wa shule ya awali wakifundishwa huku wakiwa wamekaa sakafuni na juu kukiwa wazi bila kuzekwa. Miradi mingine iliyokwama ni ujenzi wa barabara, mawasiliano ya simu, maji na umeme
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na   bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi anayemiliki shamba la mtama na uwele,ambalo Kinana alishiriki kuvuna,katika Kata ya Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika  katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala UKAWA na kutukana matuzi bungeni.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika  katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala ya UKAWA na kutukana matusi bungeni.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi.
Aliyekuwa kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akikabidhi vifaa vya ofisi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Nape na hatimaye kujiunga chama cha CCM, katika Mkutano huo wa hadhara.
Aliyekuwa kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akitupilia mbali bendera ya CHADEMA mara baada ya kutangaza kujiunga na chama cha CCM,katika Mkutano huo wa hadhara.
Sehemu ya Wakazi wa Ikungi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara.
Kinana akioneshwa bwawa la kukusanyia maji ambayo hutumika kumwagilia mashambani kwa njia ya matone.
 Wafanyakazi wa wakichuma maharage katika shamba hilo.
 Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Singida Agriculture, Ally Mohamed  jinsi wanavyomwagilia mashamba yao kwa kutumia njia ya matone kwenye shamba la kumwagilia lenye ukubwa wa ekali 200 katika Kijiji cha Mkiwa, wilayani Ikungi, Singida.
 Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Singida Agriculture, Ally Mohamed  jinsi wanavyozalisha maharage kwenye shamba la kumwagilia lenye ukubwa wa ekali 200 katika Kijiji cha Mkiwa, wilayani Ikungi, Singida.
Baadhi ya wafanyakazi wa shamba hilo wakiwa wamebeba ndoo zenye maharage hayo tayari kuyapeleka kwenda kufungasha kwenye makasha tayari kusafirishwa kwenda kuuzwa nje ya nchi.
maharage  yakifungashwa kwa ajili ya maandalizi ya kuuzwa nje ya nchi
Kinana akisaidia kufungasha maharage hayo, kwa ajili ya maandalizi ya kuuza nje ya nchi.Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Singida, Mgana Msindai pamoja na Nape Nnauye pichani kati.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...