https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, May 25, 2014

Mb Dog aendelea kufunga mkanda

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amesema baada ya kuachia video yake ya ‘Mbona Umenuna’, anaendelea na juhudi za kuwapatia raha wadau na mashabiki wake kama njia ya kuonyesha makali yake kisanaa.


Mb Dog, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema video yake imeandaliwa kwa kiwango cha juu, huku ikiwa ni sababu ya yeye kuendelea kutoa nyimbo nzuri zinazoonyesha ubora wake.

Alisema kuwa lengo lake ni kufanya makubwa zaidi katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, hasa baada ya kuamua kurudi tena katika soko hilo kwa mikakati ya aina yake.

“Nipo katika harakati za kuonyesha namna gani naweza kuonyesha ubora wangu kama ilivyokuwa mwanzo nilipotoka na wimbo wa kwanza wa Latifa, nikiwa na ‘Madee’.

“Naamini hii ni njia nzuri ya kuwapatia burudani kamili wadau na mashabiki wangu katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, hasa baada ya kuachia video yangu ya Mbona Umenuna,” alisema Mb Dog.

Mb Dog yupo kwenye harakati kabambe ya kumrudisha kileleni kwenye sanaa ya Bongo Fleva, akitokea chini ya Kampuni ya Qs Mhonda J Entertainment, yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...