Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mashabiki
wa soka wa Tanzania, leo
jioni wameondoka uwanjani kifua mbele baada ya kuishuhudia timu yao
ya Taifa, Taifa Stars, ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbawe, mechi
iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam.
Mechi
ya Stars na Zimbabwe ni ya
kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwaka 2015,
ambapo Stars imejiweka katika nafasi nzuri kabla ya mechi ya marudiano
itakayopigwa wiki mbili zijazo nchini Zimbabwe.
Bao
la Stars lilifungwa dakika ya 13 na John Bocco, huku akilifunga kwa shuti kali
nje ya 18, akitumia vyema pasi ya Thomas Ulimwengu.
Stars:
Deogratius Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub Cannavaro,
Kelvin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Jonh Bocco, Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu.
Zimbabwe:
George Chigova, Partson Jaure, Danny Phiri, Hardlife Zvirekwi, Stephen
Alimenda, Tendai Ndoro, Milton Mkude, Kudakwashe Mahachi, Cuthbert Malajila,
Peter Moyo na Eric Chipeta.
No comments:
Post a Comment