TATIZO = FURSA
ukiijua hiyo hesabu vizuri maisha kwako yatakuwa bam bam
Wasanii wengi kwa kipindi kirefu tumekuwa tunalalamika kuwa tunabaniwa kwenye MEDIA bila kuelewa kwa kifupi tu ukweli wa mambo.
Kwa Uchunguzi nilioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu hivi nimegundua
haya, Watayarishaji au watangazaji wa vipindi kwa siku wanapokea zaidi
ya nyimbo 30 kutoka kwenye studio mbalimbali hapa nchini, kwao inakuwa
ni vigumu kucheza nyimbo zote kutokana either muda kuwa mdogo wa vipindi
vyao au kuwa na request nyingi za nyimbo ambazo wamekuwa wanazicheza
sana.
Swali likaja kwangu nyimbo au video ambazo hazichezwi na ni nzuri
tufanye nazo nini ili na hawa wasanii wapate airtime?
SULUHISHO LA TATIZO
Baada ya kuliona tatizo nikapata idea ya kuzunguka kwanza Manispaa zote
ILALA, KINONDONI na TEMEKE kuangalia usajili wa vituo vya bodaboda na
bajaj zilizosajiriwa kwenye vituo ambazo pia wameweka radio ambazo
zinatumia flash na memory cards,
Huku nikapata idea ya kuanzisha KITAA RADIO ambayo itahusika na
kuwasambazia watu hapa muziki ule ambao ulishindwa kupenya radioni
muziki wa aina yeyote wa Kitanzania ambao mzuri kusikika na watu
wakaupenda.
Pili, kwenye upande upande wa video napo nikajiuliza ni mabus mangapi
yaendayo mikoani ambayo ndani hutoa burudani ya movies , music video nk
nikakuta ni zaidi ya mabus 2000 ,ambapo kwa siku kila bus linasafirisha
si chini ya abiria 50
Huku nako nikapata idea ya kuanzisha KITAA Television ambayo itakuwa
inatoa burudani ya music videos zile tu zilizokosa kupewa Airtime kwa
namna moja au nyingine
Mfanp mzuri umekuwa kwenye nyimbo ya MWANAFA ft G NAKO inakwenda kwa
jina MFALME imefanya vizuri sana mtaani na kwenye radio imeanza kwenda
vizuri sababu ya KITAA RADIO
Kwa kusema hayo machache napenda kusema KITAA RADIO na KITAA TELEVISION
imezinduliwa rasmi now chini ya kampuni ya SHOWBIZ DEFINED MEDIA Co LTD
NB ; Huduma hii tutaitoa lakini kutakuwa na uchangiaji wa huduma kwa wale watakaokuwa tayari
Aksanteni
Mike Mwakatundu
Marketing Manager
ShowBiz Defined Media Co. Ltd
showbizdefined@gmail.com
No comments:
Post a Comment