https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, May 27, 2014

Kamati ya Uchaguzi Simba yampiga chini Michael Wambura, Swed Mkwabi apeta



Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
KAMATI ya Uchaguzi ya klabu ya Simba, chini ya Mwenyekiti wake Damas Ndumbaro, imempiga chini Mgombea wa nafasi ya Urais, Michael Richard Wambura, hatua iliyomuweka katika mtego wa kuendelea na nia yake ya kuwa Rais wa Simba.
Michael Wambura, pichani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ndumbaro alisema kuwa Wambura haruhusiwi kugombea Simba kwasababu ya kosa la kimaadili, ila anaweza kukata rufaa kwa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Swed Mkwabi, pichani.
Naye Swed Mkwabi, amepita katika pingamizi alilowekewa katika mbio hizo cha Uchaguzi mkuu wa Simba utakaofanyika Juni 29. Mkwabi anawania nafasi ya Makamu wa Rais, nafasi ambayo imekuwa ngumu, ingawa mwenye anajiamini kuwa anayo sababu ya kuwa bosi wa Simba kutokana na kuungwa mkono na wanachama wengi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...