Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Uongozi wa Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa
zilizoandikwa kwenye mojawapo ya vyombo vya habari juu ya Wanachama wa Tawi la
Tandale kusema hawatambui kufutwa kwa Tawi lao.
Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, ilisema kuwa mnamo
Mei 04, 2014 Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji alitangaza kulifuta tawi hilo. Alisema uamuzi huo ulikuja baada ya tawi hilo la Tandale kutokana na
kua chanzo cha migogoro ndani ya klabu kwa kipindi cha mrefu.
Alisema kufutwa kwa tawi la Tandale unatokana na kutotimiza idadi ya
wanachama mia moja (100) kama inavyojieleza kwenye Katiba ya Yanga SC,
Ibara ya 6, kipengele cha 4
Alisema kuwa kutakuwa na uundaji wa matawi katika maeneo mbalimbali
hapa nchini na nje ya nchi, huku kiwango cha chini ya idadi ya wanachama ambao
wanaweza kunda tawi kisipungue watu mia moja (100).
“Ibara ya 13, kipengele cha 2 kinasema " Kutolipa ada zake za
uanachama kwa muda wa miezi sita mfululizo bila ya sababu maalum inayokubalika
na Kamati ya Utendaji"
“Baadhi ya Wanachama
walijifuta uanchama wao kutokana na kushindwa kulipia ada zao za
uanachana kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, kama inavyojieleza kwenye Katiba
kwamba mwanachama asipolipia ada yake zaidi ya miezi sita moja kwa moja
anajifuta uanachama wake,” alisema.
Hivyo uongozi wa klabu ya
Yanga SC unaomba umma na wanachama wake duniani kote watambue kuwa tawi la
Tandale lilifutwa kwa kutokana na kutokidhi vigezo, huku wanachama wengine sita
wakijifuta uanachama kwa kushindwa kulipia ada zao kwa kipindi cha zaidi
ya miezi sita.
Mwisho wanachama wa klabu ya
Yanga SC wanaombwa kulipia ada zao za uanchama mapema kabla ya muda wao
kumalizika ili waweze kushiriki mkutano mkuu wa marekebisho ya katiba
utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi - Oysterbay Juni Mosi 2014.
No comments:
Post a Comment