Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KOCHA wa zamani wa
Yanga, Hans van der Pluijm aliyepata timu nchini Uarabuni amekabidhiwa jukumu
la usajili wa timu hiyo baada ya yeye mkataba wake kufikia ukingoni.
Akizungumzia hilo, Mwenyekiti
wa timu hiyo, Yusuph Manji alisema Hans amewahaidi kuwaletea wachezaji wazuri. “Hans aliahidi kuleta
wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga sambamba na mridhi wake, hivyo tunasubiri
kutoka kwake.
“Pia ametuhaidi kutuletea
kocha mzuri lakini bado tuna haki ya kumkataa au kumkubali kwa maslahi ya timu
hii,”alisema.
Manji ambaye amedaiwa
kutokuwa na nia ya kuendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, alisema kwa sasa
hawana presha juu ya kupatikana wachezaji wazuri.
Alisema wamefikia
kumuani kocha huyo wa zamani wa Yanga kuwa atakuwa na nafasi nzuri ya kuwaletea
wachezaji wazuri kwa ajili ya maendeleo ya timu yao.
No comments:
Post a Comment