Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wabunge wa Upinzani, leo wameendeleza mchezo wao wa kususa na
kutoka nje ya vikao vya Bunge, kwa madai kuwa muda wa kujadili Bajeti ya Wizara
ya Nishati na Madini ni mdogo.
Wabunge wa upinzani wakati wanatoka nje ya Bunge, wakati bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini inajadiliwa.
Kauli ya kuwataka wabunge wa upinzani watoke ilitoka kwa
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, ambaye pia ndio
mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kutoka kwa wabunge hao wa upinzani kumekuwa kawaida sasa,
jambo ambalo huenda likapokewa vibaya na Watanzania.
Akizungumzia hilo mjini hapa mara baada ya kutoka nje ya Bunge, Spika wa
Bunge, Anne Makinda, alisema kuwa muda wa kujadili vikao vya Bunge la bajeti
linaloendelea ulishawekwa, ikiwa ni baada ya Bunge la Katiba kula muda wao
mwingi.
Wakati wabunge hao wanatoka nje, kauli za kejeli na dharau
dhidi yao zilisikika, ikiwa ni pamoja na waache watoke, warudishe posho na
nyinginezo.
No comments:
Post a Comment