Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya
Yanga, umesema hautasema lolote kwa sasa, licha ya kuandamwa na wimbi la
wachezaji wake wanaodaiwa kukimbilia Azam FC.
Baada ya kusajiliwa kwa Didier Kavumbagu, Azam haikutosheka
na kufanikiwa kuinasa saini ya Frank Domayo, hivyo kuongeza machungu kwa
mashabiki wake.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga,
Baraka Kizuguto, alisema kwamba hawatafungua mdomo wao kuzungumzia sakata la
kuondoka kwa wachezaji hao, badala yake wanaendelea na taratibu nyingine za
kuijenga klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya twiga na jangwani.
Alisema suala la wachezaji kusajiliwa kwa klabu nyingine ni
jambo la kaiwada, hivyo si lazima wakurupuke kutoa msimamo wao kwa kushinikizwa
na watu.
“Hatuwezi kuzungumzia chochote kwa sasa wasababu ya kuondoka
kwa wachezaji hao, maana Yanga ni klabu kubwa na yenye mipango endelevu.
“Tutazungumzia mambo yetu kwa utaratibu tuliojiwekea,
ukizingatia kuwa kuna wachezaji wengi wazuri na vipenzi vya Yanga waliondoka
nab ado timu ikaendelea kuwa imara,” alisema Kizuguto.
No comments:
Post a Comment