Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI ya muziki
wa dansi Extra Bongo Next Leval wazee wa Kimbembe inatarajia kufanya onyesho
maalumu la utambulisho wa albamu yao mpya ya ‘Mtenda Akitendewa’ kwa wakazi wa
Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga keshokutwa.
Kaimu Meneja
wa bendi hiyo Juma Kasesa, alisema kuwa ni
muda mrefu hawajatoa burudani mkoani Tanga , hivyo umefika wakati wao kutambulishwa rasmi nyimbo zao mpya zilizopo katika albamu hiyo.
Albamu hiyo imebeba
jumla ya nyimbo sita ambazo ni Mama Shuu, Ufisadi wa Mapenzi, Falsafa ya
maisha, Bakutuka Mgeni pamoja wimbo uliobeba jina la albamu Mtendwa Akitendewa.
Alisema
baada ya uzinduzi huo watawatambulisha
wanamuziki wao wapya rapa Steven Sauti ya ng’ombe na Alice waliyemchukua kutoka kituo cha
kukuza vipaji Tanzania (THT) katika kuhakikisha bendi yao inafanya kazi vizuri.
“Tuliwaahidi
wakazi wa mji wa Tanga kuja kuzindua albamu yetu kwao , hivyo tutakwenda
kukamilisha ahadi yetu pamoja na kuwatambulisha wanamuziki wetu wapya ambao
watapanda jukwaaji kwa mara ya kwanza,”alisema.
Alifafanunua
baada ya onyesho hilo watarejea jijini Dar es Salam ambapo Jumamosi watakuwa
kwenye uwanja wao nyumbani Meeda Club huku Jumapili wakiendelea na Bonanza la
Njia ya Panda ya Kunduchi.
No comments:
Post a Comment