Msimamizi wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents, Bw Tony Akwesa akitoa maelekezo kwa washiriki waliojitokeza kwaajili ya shindano la Tanzania Movie Talents kwa kanda ya Pwani unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaam
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuchukua fomu za ushiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents lililoanza rasmi leo Kwa Kanda ya Pwani.
Washiriki waliojitokeza kuchukua fomu za Shindano la Tanzania Movie Talents wakisoma fomu kwa umakini kabla ya Kujaza...
Washiriki wakipewa maelekezo na Mmoja wa wafanyakazi wa Proin Promotions
Washiriki wakisoma fomu kwa makini
Wakielekezwa Kujaza Fomu za ushiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents.
Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo Katika Kanda ya Pwani Ambapo usaili unaendelea kufanyika leo na kesho katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam ambapo takriba washiriki zaidi ya 250 wameweza kuchukua fomu za ushiriki wa Shindano hilo.
Shindano hili ni muendelezo wa shindano la kusana vipaji vya kuigiza ambalo limefanyika tayari kwa Kanda Tano za Tanzania yaani Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini na Kanda ya Kaskazini na sasa tunamalizia Kanda ya Pwani ambapo washindi watano watapatikana kwa Kanda ya Pwani na kila mmoja atajinyakulia kitita cha Shilingi Laki Tano taslimu.
Shindano hili limelenga kuibua vipaji vilivyojificha ambavyo havikuwahi kupata nafasi ya kuonekana.
Baada ya Wasindi watano kupatikana kwa Kanda ya Pwani, washindi takribani 20 kutoka kanda zote sita za Tanzania watawekwa katika kambi moja Jijini Dar Es Salaam na watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu Wa Sanaa kutoka Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo na baadae kushindanishwa na hatimaye mshindi mmoja kupatikana na Kuibuka na zawadi nono ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Vilevile Washiriki kumi watakaopatikana katika fainali hiyo watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions na watatengeneza filamu ya pamoja na hatimaye Kuweza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo.
No comments:
Post a Comment