https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Tuesday, May 27, 2014

Pigo jingine Bongo Movie Tanzania, msanii mwingine nyota afariki Dunia leo Hospitali ya Taifa MuhimbiliNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII Rachel Haule wa Bongo Movie Tanzania, amefariki Dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kutokana na matatizo ya uzazi. Rachel alifikishwa hospitalini hapo baada ya kuwa mjamzito, hata hivyo alishindwa kumka.


Taarifa iliyotumwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Chama Cha Waigizaji mkoa Dar es Salaam, leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Kaftany Masoud, alisema kwamba msanii huyo wa filamu amefariki na kuongeza pigo kwa wasanii na wadau wa filamu Tanzania.

Masoud alisema kwamba taarifa rasmi ya msiba huo itaendelea kutolewa kwa ajili ya kuweka utaratibu mzuri wa kumuhifadhi msanii huyo katika makazi yake ya milele.

Alisema msanii huyo pia mtoto wake alifariki jana hospitalini hapo na leo yeye amefariki Dunia.

“Hili ni pigo zito katika ulingo wa filamu Tanzania baada ya msanii huyu naye kufariki Dunia, ikiwa ni siku chache baada ya kumzika Adam Kuambiana katika makaburi ya Kinondoni,” alisema Masoud.No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...