Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA Cha
Netiboli Tanzania (CHANETA), kinahangaikia fedha za kuwafikisha nchini Botswana
wanapotakiwa kwenda kushiriki mashindano ya Kombe la Afrika kwa kwa timu za
Taifa za vijana, chini ya miaka 18.
Mashindano
hayo yamepangwa kuanza kutimua vumbi Juni 22 mwaka huu, ambapo timu hiyo ya
Taifa inapaswa kufika huko kati ya Juni 19 hadi 20.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Kibira, alisema kwamba
uwezo wa chama chao kifedha sio mzuri, hivyo nauli ya kuwafikisha nchini
Botswana ni changamoto kubwa.
Alisema
wanaendelea kuhaha kusaka nauli hiyo ambapo kwa pamoja timu hiyo itakuwa na
wachezaji 12 na viongozi watano, hivyo kufika idadi ya watu 17.
“Tunaomba
wadau na serikali kwa ujumla watusaidie katika hili ili tuweze kwenda
kuiwakilisha nchi kwa kupitia mashindano ya netiboli nchini Botswana.
“Haya ni
mashindano makubwa yanayoshirikisha mataifa mbalimbali ya Afrika, hivyo endapo
tutakwenda tutaiweka nchi katika nafasi nzuri zaidi kwa kupitia sekta ya
michezo, hususan hii ya netiboli,” alisema Anna.
Kwa mujibu
wa Anna, CHANETA ilianza kuwaomba wadau juu ya mashindano hayo wakihitaji
msaada wa gharama za kwenda na kurudi pamoja na posho tu, maana kula na kulala
itakuwa chini ya viongozi wa Botswana.
No comments:
Post a Comment