https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Saturday, May 03, 2014

Jengo la PCSP kugharimu Sh milioni 46Na Mwandishi Wetu, Mwanza
JENGO la Shirika Population Culture and  Sport Program (PCSP), linalojihusisha na  masuala  ya michezo na utamaduni  wilayani Nyamagana,  mkoani  Mwanza, litagharimu Sh Milioni 46 kwa ukarabati wake.

Akizungumzia hilo mjini Mwanza, Katibu Tawala wa PCSP,  Fredrick  Tingatinga,  alisema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kupanua shughuli za kijamii na michezo, ukiwamo mpira wa miguu.

Tingatinga alisema hivi sasa jengo hilo lina uchakavu hali inayorudisha nyuma mipango ya kuinua vipaji na kuendeleza tamaduni za Watanzania.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa PCSP, Juma Maiko, alivitaka vikundi vyote kujiunga na shirika hilo ili kuboresha suala la michezo hapa nchini.

Hata  hivyo ,wajumbe   walishauliwa kufanya    kazi bila mzaha ili kuboresha     suala      la  michezo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...