NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM
MSAFARA wa watu 30 wa Taifa Stars
unaojumuisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi unaondoka leo kesho
alfajiri ya Mei 29 mwaka huu kwenda Harare, Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya marudiano
ya michuano ya Afrika.
Mechi hiyo itachezwa Juni Mosi mwaka
huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare, ambapo Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itatua jijini humo saa 5 asubuhi na ndege ya Kenya
Airways.
Akizungumza leo jijini Dar es
Salaam, Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema
kuwa msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Rais wake Jamal Malinzi, ambapo utarejea
nchini Juni 2 mwaka huu.
“Wakati huo huo, mechi ya kirafiki
kati ya Taifa Stars na Malawi (Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh. 8,380,000 kutokana na watazamaji 1,504 waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo,” alisema Wambura.
Kwa mujibu wa Wambura, mgawo ulikuwa
ni kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 1,278,305.08, gharama za kuchapa
tiketi sh. 225,600, gharama za uwanja sh. 1,031,414.24, gharama za mechi sh.
1,375,218.98 na TFF/Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.
4,469,461.69.
No comments:
Post a Comment