https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, May 11, 2014

JWTZ lashiriki mkutano wa Baraza la Kimataifa la Michezo

image 

Ujumbe wa Tanzania ukiinua bendera juu kuashiria uwepo wao mkutanoni.
 
Na LuteniKanali Juma Sipe (PA, Marekani).
JWTZ limeshirikiMkutano wa Baraza la Michezo la Kimataifa (General Assembly and Congress of the International Military Sports Council -CISM) uliofanyikaMjini Quito, EquadoAmerica ya Kusinikuanziatarehe 05-09 Mei, 2014.

Mkutano huo ulijadilina kuendelea kusikiliza na ushiriki wa majeshi katika Michezo ya Kimataifa chini ya Kauli mbiu ya Baraza hilo isemayo Urafiki kupitia Michezo (Friendship through sports), msisitizo ukiwa katika kutumia michezo kama chombo cha kueneza amani na utulivu kati ya mataifa duniani.
image (1)
 
Ujumbe wa Tanzania (waliovaa sare za kijani), kutokakushoto Kanali Martin BusungunaLuteniKanali Joseph Bakariwakati wa mkutano.
image (2) 
Kanali Busungu akipiga kura wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya ya Baraza.
image (3) 
Luteni Kanali Bakari akichangia mada wakati wa Mkutano.
Badala ya kukutana na kushirikiana katika maeneo ya vita na migogoro, majeshi yakutane katika michezo na kujenga uelewano na mashirikiano yatakayopunguza uwezekano wa kuingia katika vita kama njia ya kutatua migogoro.

Moja ya mambo yaliyojitokeza katika mkutano huo ni pamoja na ushiriki mdogo wa nchi za Afrika ikilinganishwa na mabara mengine, uliodaiwa kutokana na kukosekana fedha, mwamko mdogo wa viongozi wa majeshi ya nchi husika na kutoona umuhimu wa kujenga mahusiano kupitia michezo. 

Aidha, Mkutano ulimchagua Rais mpya wa Baraza hilo, Kanali Abdul Hakeem kutoka Bahrain na Kanali Dorah Mumby (Guinea) kuwa Katibu Mkuu wa kwanza kutoka Afrika.

Ushiriki wa Tanzania na utekelezaji wa maazimio ya CISM umekuwa wa mfano kwa miaka kadha sasa. Kwa mfano,katika mkutano wake wa mwaka 2008 uliofanyika Paramaribo, Suriname, Meja Joseph Bakari (sasa Luteni Kanali) alitunukiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza hilo Nishani iitwayo ‘Order of Grand Knight’ kwa mchango wake uliopelekea kuanzishwa kwa “Twalipo Youth Sports Foundation” (twalipo soccer academy.blogspot. com) nchini Tanzania.

Katika mkutano huojumla ya wanachama 76 walihudhuria kati ya wanachama 104 wa Baraza hilo. Tanzania iliwakilishwa na Kanali MartinBusungu, Mkurugenzi wa Utimamu wa Mwili, Michezo na Utamaduni kutoka Makao Makuu ya Jeshi na LuteniKanali Joseph Bakari, Afisa mnadhimu kutoka Kurugenzi hiyo.

Mkutano huo wa mwaka hutanguliwa na mikutano ya kimabara (Afrika, Ulaya, AsianaAmerika) ambako masuala ya michezo ya Majeshi yanayogusa mabara husika hujadiliwa.kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya ushirikiano Kusini mwa Afrika nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda na Zambia.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...