https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, February 25, 2013

Tegete aumizwa na kushindwa kuiangamiza Azam FC

Jerry Tegete, kama humjui waulize Simba.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Jerryson Tegete, amesema ingawa timu yao ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC, lakini soka lake na jinsi alivyoshindwa kuifungia mabao timu yake ameumia na kuona hajajitendea haki.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Haruna Niyonzima na kupeleka shangwe kwa timu hiyo ambayo kwa sasa imefikisha pointi 39 na kushika usukani mwa ligi hiyo, ikufuatiwa na Azam FC.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Tegete alisema kwamba alikuwa na nafasi kubwa ya kuifungia timu yake mabao hata mawili, lakini bahati haikuwa yake.

Alisema jambo hilo limempa unyonge wa aina yake, akiona kuwa hajaitendea haki Yanga, ingawa walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam.

“Nashangaa kwanini nilitoka uwanjani bila kufunga hata bao moja wakati nilidhamiria na kuipania zaidi mechi hiyo, ingawa matokeo yake hayakuwa machungu kwakuwa bado sisi tulishinda.

“Matokeo ya kushinda bao 1-0 ni mazuri kwetu, lakini nilikuwa na uwezo wa kushinda, hivyo nimeumizwa kwakuwa sijaweza kuingiza bao kimiani na kututoa na ushindi mwembamba,” alisema.

Yanga ipo katika hatua nzuri ya kuweza kunyakua ubingwa wa Bara msimu huu kwa kuwapoka watani zao wa jadi Simba, ambayo yenyewe juzi ilishindwa kutoka na ushindi mbele ya Mtibwa Sugar kwa kukubali kichapo cha bao 1-0.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...