https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, February 20, 2013

Mmoja ajitoa roho baada ya kupata 'zero' kidato cha nne mkoani Tabora



Katibu Mtendaji wa Bazara la Mitihani Tanzania, Joyce Ndalichako, akionyesha moja ya karatasi za majibu zilizoandikwa uchafu na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne hapa nchini mwaka 2012.

Na Handeni Kwetu Blog
MATOKEO mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012, yaliyotangazwa mapema wiki hii, yamesababisha kifo cha Michael Fidelis, aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kanyenye, iliyopo mkoani Tabora, baada ya kujinyonga kwa kamba ya manila.

Taarifa za kujinyonga kwa mwanafunzi huyo aliyeacha ujumbe wa kutofurahishwa na zero aliyopata, imemfanya asitishe uhai wake, ikiwa  ni hatua mbaya.

Habari kutoka kwa familia ya Fidelis zinasema kwamba mara baada ya mtoto wao kujua kuwa amefeli mtihani, alichukua uamuzi huo wa kujinyonga.

Asilimia 75 ya wanafunzi wa kidato cha nne mwaka huu wamepata zero, hivyo kuleta balaa kubwa kwa wadau wa elimu hapa nchini, huku wengineo wakitaka Waziri wa Elimu, Shukuru Kawambwa ajiuzulu kwa kukwepa aibu hiyo.

Pamoja na mambo mengine, matokeo ya mwaka huu yamezikumba zaidi shule za serikali, huku watoto wa masikini ndio wakionyesha kuathirika zaidi.

Habari hii imeandikwa kwa msaada wa Clouds FM.
 

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...