https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, February 20, 2013

Mnamibia apewa ofa ya kuwania Ubingwa wa Dunia

Albinus Felesianu
Albinus Felesianu kulia akimrushia ngumi mpinzani wake kushoto.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA kijana na anayeinukia kwa kasi Albinu Felesianu wa nchi ya Namibia amepewa ofa ya kugombea ubingwa wa dunia wa Featherweight kwa vijana walio chini ya miaka 25 unaotambuliwa na IBF. 

Albinus amezoea kupewa zawadi za Christmas na siku kuu yake ya kuzaliwa lakini hamna kilichomwandaa na mshtuko mkubwa ambao aliupata wakati IBF ilipotangaza hivi karibuni kuwa imempatia nafasi ya kugombea mkanda wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25.

Mtua ambaye anaweza kuiua furaha yake ni mmoja wa watoto wa Nkrumah, Mghana Ishmael Ayeetey ambaye amekulia katika moja ya viunga vinavyosifika kwa kutoa mabingwa wa ngumi wa dunia kama kina Azumah Nelson, Joseph Agbeko na Ike Quartey.

Albinus Felesianu kulia akimrushia ngumi mpinzani wake kushoto
Mpambano huo utafanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia tarehe 29 March chini ya kampuni ya Kinda Boxing promotions ya bwana Kinda Nangolo!

Hili litakuwa pambano la pili la ubingwa wa dunia kwa vijana baada ya bondia Ilunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) kumtwanga bondia Gogito Gorgiladze wa Georgia jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini jumamosi iliyopita.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...