https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, February 06, 2013

Ally Choki asifia bonanza lao la Jumapili



Ally Choki

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, maarufu kama Wazee wa Kizigo, Ally Choki, amesema kwamba bonanza lao la kila Jumapili, linajaza watu kwasababu ya kuwasogezea burudani hizo karibu.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika viwanja hivyo vilivyopo karibu na Hospitali ya Magomeni, jijini Dar es Salaam, Choki alisema kwamba sasa mashabiki wao wameipata burudani hiyo karibu zaidi.


Alisema kila Jumapili, shoo yao hiyo imekuwa ikijaza watu wengi wanaokwenda kuangalia burudani kutoka kwa waimbaji na wanenguaji mahiri, akiwamo Rogati Hega Katapila, Ramadhan Masanja Banza Stone na wengineo wenye majina ya kutisha.

Choki alisema kwamba kwasababu hiyo wanaamini kuwa bendi yao itazidi kufanya vyema kwa kubuni mambo yenye kuleta tija katika maisha ya muziki wa dansi nchini.

“Sisi kama Extra Bongo tumekuwa kwenye mikakati ya kuweza kuwavuta au kuwasogezea burudani mashabiki wetu, hivyo naamini kwa kufanya bonanza hili la kila Jumapili, mambo yatakuwa mazuri.

“Naomba wadau na mashabiki waje kuangalia jinsi timu yangu ilivyojipanga kuanzia waimbaji hadi wacheza shoo wetu wanaongozwa na Super Nyamwela,” alisema Choki.

Extra Bongo kwa sasa inafanya vyema katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, hivyo shoo zao zote wanazofanya katika kumbi mbalimbali kupata mashabiki wengi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...