https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Thursday, February 21, 2013

Matokeo ya kidato cha nne Handeni yawaliza wadau wa elimu


Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Handeni, wakiwa kwenye ziara ya kilimo mwaka jana kabla ya mtihani wa kidato cha nne.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
AFISA Elimu Shule za Sekondari wilayani Handeni, mkoani Tanga, Simon Mdaki, amesema kwamba matokeo ya kidato cha nne wilayani kwao si mazuri, jambo linalowafanya waendelee kujipanga kukabiriana na changamoto hizo.

Matokeo ya kidato cha nne Tanzania yalitangazwa mapema wiki hii, huku asilimia kubwa wanafunzi wake wakiwa wamepata ‘zero’.

Akizungumza na Handeni Kwetu jana, Mdaki alisema kwamba wilaya yao ina changamoto nyingi, ikiwamo upungufu wa walimu, madarasa na vifaa vya kufundishia, jambo linalowapa wakati mgumu katika kiwango cha elimu.

Alisema wanajitahidi kuangalia kwa kina matokeo hayo kwa ajili ya kufanya vyema katika siku zijazo, kwa kuhakikisha kuwa zile dosari zinazojitokeza wanapambana nazo.

“Matokeo si mazuri kwa shule za sekondari wilayani kwetu, maana watoto wamefeli sana, ikiwa ni sababu ya ukosefu vifaa vya kufundishia na mambo mengine.

“Ni matokeo ambayo sisi wote yanatuumiza kichwa, hivyo nadhani tuna wajibu wa kujipanga katika hali ya kutoka hapa tulipokuwa sasa na kuipaisha wilaya katika suala zima la elimu,” alisema Mdaki.

Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 ni janga la Kitaifa, baada ya wanafunzi wengi kuanguka hasa wanaosoma katika shule za serikali, zikiwapo zile za Kata ambazo ndio nyingi na zinazotumiwa na watoto wengi wa masikini.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...