https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, February 20, 2013

KIJANA OMBENI MBEULA ANAHITAJI MSAADA WA HALI NA MALI ILI AWEZE KUPATA MATIBABU HARAKA.SAMAHANI KWA HIZI PICHA
 
 Ombeni Mbeula akiwa amekaa kitandani ndani ya hospitali ya mkoa wa Dodoma
 Huyu ndio mama wa mtoto Ombeni Mbeula anaitwa Kilaudia Kigaila
Huu ndo mwonekano wa mtoto Ombeni Mbeula akiwa amelala hospitalini
 Mama wa mtoto Kilaudia Kigaila akiwa na mwanae Ombeni Mbeula
Nyumba iliungua wakati watoto hao wamekaa ndani na wakati huo huo mama wa mtoto alikuwa amekwenda shambani maeneo ya Chitemo iliyoko wilaya ya mpwapwa
 
Wakati mvua inanyesha ghafla nyumba ilibomoka na wakati huohuo walikuwa watoto wawili walikuwa jikoni ndani ya hiyo nyumba. Baada ya tukio hilo kutokea   ikafanyika uokoaji kwenye nyumba hiyo maeneo ya Chitemo na kufanikisha   kuokoa watoto wote wawili kati ya mmoja aliumia kwa kuangukiwa na udongo wa nyumba hiyo na huyu Ombeni Mbeula aliangukia kwenye moto mpaka kuungua hivi unavyoona kwenye picha lakin hali zao ni salama kwa wote.
 
Baada ya uokoaji waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospitali ya Mima iliyoko Mpwapwa ikashindikana madaktari wakamuagiza aende hospitali ya Mpwapwa hapo hospitalini wakakaa siku mbili katika hospitali ya mpwapwa  na siku ya tatu wakaambiwa waende hospitali ya rufaa iliyoko Dodoma Mjini ambayo ni inajulikana General kwa matibabu zaidi.
 
Walipofika katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wakaanza matibabu lakini uwezo wa kipato cha wazazi wake sio kizuri inahitajika msaada kwa matibabu maana hata dawa hajapatiwa na pesa kwa ajili ya matibabu  haikuweza kupatikana paka sasa
 
Kama umeguswa kutoa ni moyo sio utajiri muokoe mtoto huyu maana hata kula anashindwa mpaka kuona anaona kwa mbali sana.
 
Mama yake hana simu lakini anatumia simu ya  ndugu yake Ekiria Paskali
 
Kwa yeyote atakayependa kumchangia mtoto huyo atume chochote kwenye namba hii au atumie M- pesa kwenye namba hii 0757 498336. PICHA KWA HISANI YA PAMOJAPURE BLOG

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...