https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, February 15, 2013

Lowassa akerwa na vurugu za Buserere, mkoani Geita


Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mchungaji Trafaina Aseri Nkya ambaye pia ni msaidizi wa Askofu Mteule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria na ujumbe wake walipofika nyumbani kwake eneo la Ngarashi kijijini kwake Monduli, kumshukuru kwa harambee ya ujenzi wa kanisa lao aliyoiendesha Januari mwaka jana na kupatikana kiasi cha shilingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi.

Ujumbe wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo ukimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward 


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasindiki zawajumbe hao.
 
Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa, amewataka vingozi wa dini nchini, kusaidia na kurejesha hali ya amani kati ya wasilam na wakiristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.

Akizungumza hayo nyumbani kwake Monduli, wakati alipokuwa akipokea ujumbe kutoka kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa amesema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buserere, yanasikitisha sana na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.

"Rais ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba viongozi wa dini na madhehubu yote wasimamie na kuzuia mambo haya, nawaomba watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu isipotee," alisema.

Katika fujo hizo za Buserere,mchungaji mmoja wa kanisa la sabato aliuwawa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya waislam na wakristo.Chanzo cha mapigano hayo kilikuwa ni wakristo kuamua kuchinja ng'ombe na kuuza kwenye bucha lao, hatua iliyopingwa na wananchi wa dini ya kiislam kwenye eneo hilo.

Ujumbe huo uliyofika nyumbani kwa Mh Lowassa ukiongozwa na msaidizi wa askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki mwa ziwa victoria, ulifika kumshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa kuu la Shinyanga January mwaka jana ambapo zaidi ya shillingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...